ZION TRANSFORMATION CHILDREN CENTER

zb

zb

Friday 2 September 2016

IFAHAMU HUMASA



Kituo cha Huduma ya mabadiliko ya mtoto kimeazishwa rasmi mwaka 2016, kikiwa ni kituo ambacho kinasajili watoto wenye mahitaji mbalimbali ya kiroho na kimwili bila kujali Dini, kabila, au jinsia zao ili kumhudumia mtu katika ukamilifu wake. Nia ni kuhakikisha kuwa mtoto na familia yake kitaifa na kimataifa wanafikiwa na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu kwa watu wote, ili wafanyike kuwa waumini wanaomwabudu Mungu katika roho na kweli.

Taratibu za Kituo cha Huduma ya mabadiliko ya mtoto zimeandikwa katika katiba na ndizo zitakazotumika katika kuongoza kituo hiki kama mwongozo wa kituo katika mambo yote yanayohusu uendeshaji wa kituo na utoaji wa Huduma.

Kituo hiki si cha kibiashara na kimeanzishwa kwa nia ya kutangaza upendo wa Mungu kwa kusaidia watoto wahitaji.

1.1        JINA LA KITUO NA MAKAO MAKUU


(a)  Jina la Kituo litakuwa “ZION TRANSFORMATION CHILDREN CENTER” KWA KIFUPI (ZITRACC) au kwa Kiswahili
“HUDUMA YA MABADILIKO YA MTOTO SAYUNI” (HUMASA)
(b)  Logo ya kituo itakuwa kama inavyoonekana hapa chini:

                                            

(c)  Makao makuu ya Kituo yatakuwa Wilaya ya Musoma, mkoani Mara katika Kata ya Kwangwa mtaa wa Kiara.

0 comments:

Post a Comment