UONGOZI WA KITUO CHA HUDUMA YA MABADILIKO YA MTOTO SAYUNI (HUMASA)
Kituo cha Huduma ya Mabadiliko ya Mtoto Sayuni ni kituo kilichoanzishwa kutokana na wito wa ndani wa watumishi wa Mungu kuhusu namna ya kuwahudumia watoto wahitaji na hasa katika kubadili mtazamo wao wa jinsi jamii inayowazunguka inavyowatazama na kuwaona! uongozi wa kituo umechukuwa dhima hii muhimu kuhakikisha kuwa watoto hawa wanapata mabadiliko ya kweli Kiroho, kifikira, na kimwili ili wawe watu wazima baadaye watakaoisaidia familia, jamii inayowazunguka na hatimaye taifa.
Katika Maandiko Matakatifu Israel anakumbushwa kuwa Maskini wapo katika Israel ili yeye Israel awahudumie! Ndiyo kusema hata leo sisi tupo katika mazingira tofauti tofauti ili kuhakikisha kuwa wahitaji wanahudumiwa. Hivyo basi ni jukumu letu sisi kama kituo kuhakikisha kuwa watoto wahitaji tutakaowabaini wanahudumiwa kwa kadri ya uwezo tutakaokuwa nao. Na tunaomba sana sisi kama Staff kuwa hatutafika mahali tusahau huduma hii muhimu tuliyopewa na Mungu wetu. Hivyo ni wajibu wetu kuhamasisha raslimali zilizopo ndani na nje ya nchi ili kuwahudumia watoto wahitaji katika uhitaji wao huku tukijua kuwa wao ni wa thamani sana kwani wameumbwa kwa sura na mfano wa Mungu!
Hapa chini ni Uongozi wa Kituo uliobeba Maono haya Muhumi:
MWENYEKITI WA KITUO
MHAZINI WA KITUO
WAJUMBE
1.
2.








Hongereni sana kwa kazi hii kubwa muifanyayo! Bwana na awabariki sana!
ReplyDelete