HUMASA Management team on day one as we were opening the center program today! We wish you all the best and the almighty God be with you! Amen. |
HUDUMA YA MABADILIKO YA MTOTO SAYUNI
Hii ni huduma ya kipekee kutoka kwa Mungu Baba aliyeweka mzigo wa kuwahudumia watoto wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi na pia yatima na wale wote ambao kipato chao ni cha chini sana kiasi kwamba wanakosa mahitaji na huduma muhimu katika maisha yao.
Kituo kinakusudia kuwalea watoto katika maadili mema ya upendo na kumjua Mungu wa kweli katika maisha yao bila kubagua dini, jinsia, au kabila la mtoto. Na tutakuwa miongoni mwa vituo bora kabisa nchini vinavyotoa huduma kamilifu kwa watoto wahitaji.
Maono yetu ya mbele ni kuona watoto hawa wakiwa katika hali bora kabisa katika nyanja mbalimbali aidha ya ajira ya kuajiriwa au kujiajiri lakini pia wajasiriamali wakubwa watakaoleta mabadiliko ya kweli katika nchi hii.
Huduma ya mabadiliko ya mtoto inakusudia kumlea mtoto katika makuzi mema ambapo atamuona Mungu na upendo wake kwa wahitaji ukibdilisha maisha yake.
Ni maombi yangu Mungu wa Mbinguni atafanya alilolikusudia ktika kituo hiki na kwa imani tunaona makubwa mbele yetu. Mungu awazidishie staff wote baraka na maono ya kuiinua na kuipeleka huduma hii
mahali panapotakiwa! Ameni.
MALENGO YA KITUO:
1.
KUHUSU ELIMU
Kuhusu elimu ya
mtoto kituo kitahakikisha mtoto aliyeko kituoni anapata elimu bora katika shule
anayosoma. Hivyo katika kusimamia hilo kituo kitafanya yafuatayo katika sekta
ya elimu:
- Kuhakikisha kuwa matokeo yote ya mtoto yanaletwa kituoni
- Kumwezesha mtoto kupata vifaa vya kijifunzia kama daftari, kalamu na uniform za shule
- Kumtia moyo mtoto kufanya vizuri katika masomo yake baada ya kujua maendeleo yake
2.
KUHUSU AFYA
Kwa upande wa
afya kituo kitahakikisha kuwa mtoto anakuwa na afya njema kwa kupata huduma
mbalimbali zitakazoboresha afya yake kama vile:
- Kuhakikisha kila inapowezekana mtoto anapata lishe bora japo mara moja kwa wiki kituoni
- Kutoa huduma ya matibabu kwa mtoto anapougua
- Kwamba mtoto wa kituo anapata nafasi ya kuingizwa katika mpango wa bima ya afya (CHF)
3.
KUHUSU HUDUMA YA
KIROHO
Kituo
kinakusudia kuzalisha jamii bora itakayofaa kwa kizazi hiki cha sasa kwa kuhakikisha
kuwa mtoto wetu kituoni anakuwa mfano wa kuigwa katika jamii aishio kwa tabia
njema, heshima, maadili, na hofu ya Mungu ndani yake. Hivyo kituo kitafanya
yafuatayo upande wa kiroho:
- Kuhakikisha kuwa mtoto anafundishwa neno la Mungu kila tunapokutana kituoni
- Kutoa vifaa na machapisho yatakayofaa ili kumwendeleza zaidi kiroho
4.
KUHUSU MAMBO YA
KIMWILI
Katika eneo hili
kituo kitahakikisha kuwa mtoto aliyesajiliwa kituoni anapata huduma mbalimbali
kuhusu mwili wake. Hii ni kumaanisha kuwa kituo kitafanya yafuatayo upande wa
huduma ya kimwili:
- Mtoto anapata fursa ya kujiendeleza katika stadi za maisha na ujasiriamali.
- Kupata vifaa mbalimbali katika kuuweka na kuutunza mwili wake katika hali ya usafi daima.
5.
KUHUSU MICHEZO
Ili kuimarisha
miili yao na kuwa na afya bora pia katika suala zima la kubaini na kuendeleza kipaji
cha mtoto tunaamini ni lazima mtoto apate nafasi ya kucheza. Hivyo kituo
kitafanya yafuatayo katika kuhakikisha lengo hili linafikiwa:
- Kila mtoto atatiwa moyo katika kipaji anachoamini kuwa nacho
- Kituo kitabaini na kuendeleza kipaji cha mtoto katika maeneo mbalimbali kama vile:
o
Uimbaji
o
Uigizaji
o
Mpira wa miguu
o
Mpira wa pete
o
Riadha n.k.
Kwa neema ya Mungu tunaamini Mungu
ana makusudi makubwa na watoto hawa na hivyo tunaamini kuwa malengo haya
yatafanikiwa kwa kadri Mungu mwenyewe atakavyokuwa akitupa neema zake
kituoni.
AMENI NA KARIBU SANA
Iwapo
utakuwa umeguswa na huduma hii tafadhari wasiliana nasi kwa contacts zetu
zilizopo katika blog hii kwa mawasiliano zaidi. Barikiwa sana na Mungu wa
Mbinguni.
0 comments:
Post a Comment