KARIBU KWENYE SIKU YA FURAHA HAPO KESHO
Zawadi James Mussa (Executive Committee Member) |
Mpendwa msomaji wa blog hii ya HUMASA! Ni siku nyingine njema ambayo Mungu ameifanya ili tufurahie uzuri wake maishani mwetu. katika mojawapo ya makala zilizoandikwa katika blog hii ilihusu siku ambayo watumishi wa kituo watapita huko Kwangwa kwenye mitaa ya Kata hiyo kuwabaini watoto wahitaji tayari kwa huduma iliyokusudiwa kwao.
Napenda kukujulisha ndugu msomaji kuwa kesho timu nzima ya Zitracc au wana Humasa wakiongonzwa na Mjumbe wa Kamati kuu ya HUMASA (Zawadi James pichani) watakuwa wakipita na kubaini watoto watakaojumuishwa katika kituo hiki cha mabadiliko ya mtoto Sayuni. kazi hii ni ngumu lakini tunatazamia Mungu atatusaidia kuifanya kwa ufanisi na weredi mkubwa ili kuwabaini na kuwapata watoto ambao kweli watakuwa na uhitaji ili waone upendo wa Mungu katika maisha yao!
MUNGU ANAITWA BABA WA YATIMA NA PIA ANAITWA MUME WA WAJANE! HII NI KWA SABABU UMSAIDIAPO MUHITAJI UNAGUSA MOYO WA MUNGU! UNALIJUA HILO?
KARIBU KITUONI MTOTO NA MLEZI KWA MAISHA MEMA NA YENYE ADILI NA YALIYO PIA NA HOFU YA MUNGU NDANI YAKE. ASANTENI SANA NA KARIBUNI TENA!
0 comments:
Post a Comment