Ni kweli kabisa kumekucha! Kwa nini kumekucha? Ni wiki kesho tu inayoanza tarehe 12/09/2016 katika mitaa ya Kata ya Kwangwa wana Zitracc au ukipenda Humasa kwa lugha yetu adhimu ya Kiswahili wakiwa Jopo zima watakuwa wakizunguka kuwabaini watoto wahitaji 50 kwa kuanzia!watakaopata fursa wa kuwa watoto waanzilishi wa kituo! kwani watakuwa wakisajiliwa. Muda na siku ya kupita mitaani mtajulishwa!
Usingependa upitwe na nafasi hii muhimu kukua na kulelewa katika kituo hiki cha Mabadiliko ya Mtoto! Hivyo hakikisha unakuwepo nyumbani ili usipitwe na fursa hii adimu! Ni matumaini yetu kuwa Mungu atatujalia kufika salama salimini katika siku hiyo muhimu tayari kwa kukutana Jumamosi ya kwanza Pale sehemu muhimu, tulivu, na yenye hewa na upepo mwanana.
Si pengine bali ni pale makao yetu makuu ya Kituo kama yanavyoonekana pichani. Kidhi vigezo, kuwa mwaminifu na Karibu Kituoni
KARIBU KITUONI UONE NA UHISI UPENDO WA MUNGU KWAKO
Tunawapenda na kuwakaribisha wote! Karibui
ReplyDelete