WATOTO KWA MUNGU YOTE YAWEZEKANA HAKUNA KUKATA TAMAA!
Duniani kuna vitu vingi vigumu! Si vigumu kwa maana ya ugumu wa kitu unapokibonyeza lakini ni katika kujaribu kukielewa au kukifanya. Yapo mambo magumu mengi katika dunia hii na wakati mwingine binadamu huyaona rahisi kabla ya kuyafanya au kumfika yeye!
Waweza kufurahia na hata kuwaona wengine hawafai pale umwonapo Messi au Ronaldo akiwapita mabeki zaidi ya wanne hadi kufunga goli kwa ustadi na ukadhani imetokea tu ikawa hivyo. Si rahisi kiasi hicho kuna muda wa kutosha ambao watu hawa huutumia katika "trainning" na hata pale umwonapo Bolt akiwaacha wenzie mara kwa mara anakuwa kafanya kazi ya ziada mazoezini hadi kufikia kiwango hicho.
Ninachotaka kusema hapa ni kuwa Sisi kama kituo tutawatia moyo vijana na watoto kituoni kujaribu vitu hata vile ambavyo mwishoe vimekuwa kama janga la kitaifa. Mojawapo ya masomo yanayowasumbua sana vijana wetu ni masomo ya Sayansi. Tutawatia moyo watoto na vijana kuhakikisha kuwa hata vile vitu vinavyoaminika kuwa vigumu vinawezekana!
Na tunaamini kwa msaada wa Mungu itawezekana kwani katika maandiko twasoma kuwa:
"NAYAWEZA MAMBO YOTE KATIKA YEYE ANITIAYE NGUVU!"
0 comments:
Post a Comment