ZION TRANSFORMATION CHILDREN CENTER

zb

zb

Sunday, 9 October 2016

WATOTO WAKIWA KATIKA FURAHA YA MICHEZO BAADA YA VIPINDI KITUONI

Pamoja na vipindi vifundishavyo mambo ya kiroho, usafi wa mwili, mambo ya ufahamu kwa ujumla mwisho wa siku watoto huviweka viungo vya miili yao sawa kwa michezo mbalimbali kituoni Tazama picha hapa chini

Wasichana wa darasa la Yerusalemu wakiwa kituoni kwa furaha baada ya kumaliza vipindi na kuingia katika michezo.
Wavulana wa Darasa la Yerusalemu nao hawakubaki nyuma baada ya vipindi walijiburudisha kwa kucheza mpira wa miguu. tunawatia moyo watoto kituoni kubaini vipaji na kuwasaidia kuviendeleza.
Hawa ni Darasa la Emmaus nao kumbe wanaujua mpira! wamejipanga tayari kwa kulisakata kabumbu.

Darasa Eden wao pamoja na mpira na michezo mingine hawakusahau daftari zao! wanaamini katika kumshika sana Elimu wasimwache aende zake lakini pia ni lazima wacheze ili kuiweka sawa miili yao! 
KWA UJUMLA TUNAMSHUKURU SANA MUNGU KUTUJALIA KATIKA KUWALEA WATOTO HAWA. TUNAAMINI TUNAFANYA KAZI NJEMA KATIKA UFALME WA MUNGU NA NI AGIZO LA MUNGU KUTUTUMIA MIMI NA WEWE KUUNGANA KATIKA JUKUMU HILI. BASI KARIBUNI KWA MAWASILIANO ZAIDI NA HATA KUTUTEMBELEA ILI KUWATIA MOYO WATOTO HAWA ILI WAUONE UPENDO WA MUNGU KATIKA MAISHA YAO!

0 comments:

Post a Comment