Mwanzo 2:8,9,15
MAZINGIRA HOYEE! NI MPANGO WA MUNGU
Ukitazama mistari hii ya Biblia utagundua kuwa Mungu wetu ni wa ajabu sana na hupanga mipango yake kwa weredi wa hali ya juu. nasema hivi kwa sababu utaona katika mistari hii Mungu pamoja na kumuumba mtu kwa mfano na sura yake bado aliona ni vizuri kumwandalia mazingira huyo aliyemuumba.
Hivyo baada ya uumbaji mwingine wote Mungu anaandaa maZingira ambayo kwayo mwanadamu ataishi na aifurahie dunia. Ndiyo kusema kwa lugha rahisi katika sayansi ya Mungu, Mungu aliona ili binadamu aishi vizuri na aifurahie dunia ni lazima amwandalie mazingira mazuri atakayoishi ndani yake!
Jambo la kutisha ni kuwa wakati mwingine mwanadaMu huyu aliyewekewa mazingira mazuri na Mungu mwenyewe huyaharibu mazingira hayo yeye mwenyewe kwa mikono yake! Tumeshuhudia uchomaji wa misitu, uharibifu wa mazingira kwa kuharibu ardhi na maji kwa madawa na kemikali nyingi na kali! uuaji wa viumbe vya msituni majini na ardhini kwa sumu na uharibifu mkubwa usiositahili nk. nadhani Mungu aonapo haya hutushangaa sana.
Pengine swali la kujiuliza ni kuwa wewe binafsi unafanya nini katika kuenzi ubunifu alioufanya Mungu mwenyewe katika kuhakikisha kuwa mazingira yanatunzwa?
NI WAJIBU WETU KUTUNZA MAZINGIRA KWANI KWA KUFANYA HIVYO TWAMTUKUZA MUNGU! WAJIBIKA
0 comments:
Post a Comment