Kituo cha Huduma ya mabadiliko ya mtoto kimeazishwa
rasmi mwaka 2016, kikiwa ni kituo ambacho kinasajili watoto wenye mahitaji
mbalimbali ya kiroho na kimwili bila kujali Dini, kabila, au jinsia zao ili kumhudumia mtu katika ukamilifu
wake. Nia ni kuhakikisha kuwa mtoto na familia yake kitaifa na kimataifa
wanafikiwa na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu kwa watu wote, ili
wafanyike kuwa waumini wanaomwabudu Mungu katika roho na kweli.
Taratibu
za Kituo cha Huduma ya mabadiliko ya mtoto zimeandikwa katika katiba na
ndizo zitakazotumika katika kuongoza kituo hiki kama mwongozo wa kituo katika
mambo yote yanayohusu uendeshaji wa kituo na utoaji wa Huduma.
1.1 JINA LA KITUO NA MAKAO MAKUU
(a) Jina
la Kituo litakuwa “ZION TRANSFORMATION CHILDREN CENTER” KWA KIFUPI (ZITRACC) au
kwa Kiswahili
“HUDUMA YA MABADILIKO YA MTOTO SAYUNI”
(HUMASA)
(b) Logo
ya kituo itakuwa kama inavyoonekana hapa chini:
(c) Makao
makuu ya Kituo yatakuwa Wilaya ya Musoma, mkoani Mara katika Kata ya Kwangwa
mtaa wa Kiara.
0 comments:
Post a Comment