ZION TRANSFORMATION CHILDREN CENTER

zb

zb

Sunday, 4 September 2016

KUWAWEZESHA WATOTO KUINUA VIPAJI VYAO

Mojawapo ya mambo ambayo kituo kitafanya ni pamoja na kuvumbua kipawa na kipaji cha mtoto. tunaamini katika ulimwengu huu wa sasa vipaji na vipawa ni muimu sana kwani ni ajira pia kwa vijana wenye vipaji.

Tunaamini na tungependa vijana wetu wote wasome hadi elimu ya juu. Lakini mara nyingine si rahisi na si njia pekee ya kumtoa mtu kimaisha hasa katika ulimwengu huu wa sasa wenye wasomi wengi wasio na ajira! hivyo basi pamoja na kuwahimiza kwa kasi na kwa nguzu zetu zote kuhusu umuhimu wa elimu hatutasahau pia kuinua vipaji na vipawa vyao ili kuwa watu muhimu katika familia zao, jumuiya waishizo lakini pia Taifa kwa ujumla wake.

NDO MAANA NIKASEMA "KONGOLE" KIJANA KWA KUTAMBUA KIPAJI CHAKO


MUNGU AKUKUZE HUKU UKIMJUA YEYE NA AZIDI KUKUBARIKI UNAPOENDELEA NA MASOMO YAKO PIA. AMEN!

0 comments:

Post a Comment