Katika hali ya kumshukuru Mungu kituo cha Humasa kilichoanza hivi karibuni katika kata ya Kwangwa kwa neema ya Mungu kimeweza kuwapatia watoto wote kituoni sare za kituo watakazozitumia wakati wakija kituoni na kwenye matukio maalumu. Tukio hilo limefanyika leo 15/10/2016 hapo kituoni ambapo Mwenyekiti na watendakazi wote wa kituo walikuwepo kushuhudia tukio hilo muhimu.
Wazazi na walezi wenye watoto kituoni walikuwepo kushuhudia watoto hawa wakipokea sare hizo na kuleta hali ya furaha kubwa! Ni matumaini ya Kituo kuwa wazazi watashirikiana bega kwa bega na Kituo katika kuhakikisha kuwa yale yote yaliyomo katika mpango wa mwaka huu yanakamilika!
Fuatilia picha hizi hapa chini kujionea jinsi hali ilivyokuwa kituoni:
|
VIONGOZI WAKIWA KIKAZI ZAIDI KATIKA KUHAKIKISHA ZOEZI LINAFAULU VIZURI |
|
WATUMISHI KITUONI WALIFANYA KAZI KUHAKIKISHA KILA KITU KIMEENDA SAWA |
|
WAZAZI NA WATOTO WAO KATIKA PICHA KITUONI |
|
UTARATIBU MAALUMU ILITUMIKA KUHAKIKISHA KUWA KILA ALIYECHUKUA SARE ANAREKODIWA |
|
MAMA NA MWANAYE KATIKA HALI YA FURAHA BAADA YA KUPATA SARE YA KITUO |
|
WATOTO WOTE KITUONI KATIKA PICHA YA PAMOJA WAKIWA WAMEVAA SARE ZAO |
|
BAADHI YA SEHEMU YA WATOTO KATIKA PICHA YA PAMOJA |
|
BAADHI YA SEHEMU YA WATOTO KATIKA PICHA YA PAMOJA |
|
ILIBIDI MWONEKANO WA NYUMA NAO UTAFUTWE! WATOTO HAWA BWANA!! |
|
WATOTO WAKITOKA KITUONI KWA FURAHA BAADA YA KUPEWA SARE YA KITUO |
|
VIONGOZI WA WA KITUO NAO HAWAKUBAKI NYUMA |
|
DARASA LA EDENI KATIKA PICHA YA PAMOJA |
|
HAWA NI "WAZEE WA KIJIJI" YERUSALEMU |
|
EMMAUS PIA WALIKUWEPO KUPOKEA SARE ZAO |
|
|
|
MWENYEKITI KWA NIABA YA KITUO ANAPENDA KUWASHUKURU WADAU WOTE KATIKA KUFANIKISHA ZOEZI HILI. SHUKRANI ZIWAFIKIE PIA WAZAZI KWA KUTUTIA MOYO KWA KAZI NZURI TUNAYOIFANYA! TUNAAMINI MUNGU YUKO UPANDE WETU KWANI MAANDIKO YANAUNGANA NASI KUWA NI JAMBO JEMA KUWAHUDUMIA WAHITAJI NA KUWA HII NDIYO DINI YA KWELI! HEBU KUBALIANA NA MUNGU MWENYEWE KATIKA KUKIINUA KIZAZI HIKI ILI TUWE NA TAIFA LIFAALO MBELENI.
KWA MSAADA ZAIDI INGIA KATIKA BLOG YETU NA UENDE ENEO LA CONTACTS MAHALI HAPO UTAPATA KILA UNACHOHITAJI ILI KUUNGANA NASI KATIKA KUWASAIDIA WATOTO! KARIBU TUFANYE MAPENZI YA MUNGU!!
0 comments:
Post a Comment